Fahamu makosa ya KickAssTorrents kufungiwa

Mtandao wa KickassTorrents ambao ni mmoja
kati ya mitandao mikubwa ya kusambaza filamu,
miziki na program za kompyuta umefungwa leo
na pia Artem Vaulin (30) anayetuhumiwa kuwa
ndiye mmiliki wake amekamatwa na maafisa wa
Marekani akiwa nchini Poland.
Anuani nyingi ambazo zilikuwa zinatumiwa na
mtandao huu zimeanza kufungwa ingawa zipo
baadhi mpaka wakati wa kuandika makala hii
zilikuwa zinafanya kazi. Pamoja na kuzifunga
anuani za mtandao huo maafisa hawa pia
wanafanya mpango wa kumsafirisha Artem
Vaulin kwenda marekani ili akashitakiwe huko.
Kwa wasioijua KickassTorrents (Torrenting)
Torrenting ni itifaki ama protocol ama unaweza
kuuita njia ya kushirikishana mafaili kati ya
kompyuta na kompyuta, KickassTorrents na
mitandao mingine ya kiharamia inatumia
teknolojia hii kusambaza nakala hata za filamu
miziki na programu za kompyuta ambazo zina
haki miliki bila ya gharama yeyote.
Soma Pia – Fahamu jinsi ya kudownload vitu
kupitia mfumo wa Torrent
Kwa wapenda filamu na miziki hapa ndio
imekuwa mahara pa kupata mahitaji yao ya
muziki filamu na hata programu za kompyuta
huduma hizi zinatolewa na mitandao mingi lakini
mpaka miaka ya karibuni KickassTorrents ilianza
kushika kasi baada ya mtandao uliokuwa juu
kupata matatizo kama haya yaliyowakuta
KickassTorrents.
Makosa aliyoyafanya Artem Vaulin yaliyomfanya
ashtukiwe na maafisa wa Marekani na
kukamatwa
Kwanza Artem alitumia anuani yake katika
soko la muziki la iTunes anuani hii ndiyo
aliyokuwa anatumia katika kuendesha
mtandao huu.
Alikuwa anatumia kompyuta moja kuingia
iTunes na pia katika ukurasa wa Facebook
wa Kickasstorrents kitu ambacho
kilithibitisha kwamba lazima mtumiaji wa
akaunti ya iTunes atakuwa ndiye mmiliki
wa mtandao huu
Username “Nike” aliyokuwa anaitumia
kuingilia katika servers za
KickassTorrents ndiyo ilikuwa username
katika mtandao wake wa kuchat kipindi
cha nyuma.
Artem alikuwa amejiandikisha iTunes kwa
barua pepe ya tirm@me.com lakini
inajulikana wazi kwamba “tirm” ni
username ya mtawala (administrator) wa
Kickass
Pengine kukamatwa kwa Artem Vaulin kwa
namna moja kunaweza kugeuza mtazamo wa
watu kwa kampuni ya Apple ambayo ilitoa
taarifa za kijana huyo baada ya kuombwa na
maofisa usalama wa Marekani. Miezi michache
nyuma ilionekana kinara wa kutunza siri za
wateja wake.

Previous
Next Post »

2 comments

Write comments
Riwade
AUTHOR
23 July 2016 at 20:43 delete

Hatari sana hiyo.

Reply
avatar
Unknown
AUTHOR
24 July 2016 at 00:07 delete

Hiyo kitu balaaa sana

Reply
avatar

Ads Inside Post