Tukae Mkao Wa Kula Kwa Ajili Ya ‘Voice Mail’ Katika WhatsApp!

Toleo lililotolewa la kwa ajili ya majaribio la
WhatsApp katika vifaa vya Android linahusisha
kipengele cha Voice Mail
Voice Mail ni uwezo wa mtu wa kuacha ujumbe
wa sauti wakati akiwa anakupigia simu. Simu
yako inaweza ikawa haipatikani au ikawa
haipokelewi basi mtu akawa ana uwezo wa
kuweza kukuachia ujumbe flani hivi wa sauti
Kutokana na kwamba WhatsApp wamehusisha
kipengele hicho katika toleo lao la majaribu basi
sio siri tena kuwa kipengele hicho kipo njiani
kupatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp
Kwa wale ambao wapo katika programu spesheli
ya watumiaji wa kujaribu baadhi ya App za
Android (Android Beta Testing Program) ndio
wamekuwa watu wa kwanza kabisa katika
kukijaribu kipengele hiki
Toleo namba 2.16.189 la App hiyo ndio
limeongezewa hiki kipengele. Mtu unaweza
ukasema kuwa ‘aaaah Voice mail kwanza
zimepitwa na wakati’ lakini kumbuka huduma hii
inaweza ikawa ni ya muhimu sana kwa mfano
kama unaongea na wafanya kazi wenzio nje ya
nchi
Baada ya simu kukatwa (bila kuongea) au
kutopokelewa kabisa kuna machaguo yatatokea
katika simu janja yako. Machaguo yatakuwa ni
Cancel out of the menu, call back , record voice
message sasa hiyo ‘record voice messege’ ni
sawa kabisa na kuacha ‘voice mail’
Tukae mkao wa kula kwa ajili ya kusubiria
kipengele hiki katika simu zetu. Lakini hapa cha
muhimu kutilia maanani ni kwamba kwa kuwa
bado huduma hii inafanyiwa majaribu hivyo
haimaanishi kuwa itakuja latika vifaa vyetu
dhahiri. Yaani tusiwe na asilimia mia moja kwani
kitu kinachofanyiwa majaribio kinaweza kisifaulu
pia

Previous
Next Post »

Ads Inside Post