Najua ushawahi
kujiuliza ni jinsi gani
utaweza
kushusha /’download’
vitu mbalimbali kama
nyimbo, tamthilia
flani unazofuatilia na
unapata shida kuziona, makala flani
(documentary), au ata filamu flani, vitu ambavyo
vanaweza kuchukua muda mrefu kuvi’download
kwa kawaida.
Tena ukiangalia suala la mwendo (speed) mdogo
wa intaneti hili linakuwa kikwazo, kwani
unaweza ukaanza alafu intaneti ikasuambua
wakati hata unakaribia kumaliza. Hapa ndo
umuhimu wa kutumia mfumo wa ‘torrent’ katika
kushusha mafaili makubwa kwa madogo unakuja.
Mfumo huu ni wa umoja katika kushusha kitu,
yaani ukianza kushusha faili flani utakuwa
unashusha kutoka kwa watu wengi yaani hata
maelfu. Fikiria hivi, unandoo na unachota maji,
kwa mfumo wa kawaida utakuwa unachota moja
kutoka kwenye bomba moja, ila kwa mfumo wa
torrent ni sawa na kuchota maji kutoka mabomba
mengi kwa wakati mmoja. Hii inasaidia kuongeza
mwendo wa intaneti katika kushusha, na faida
nyingine ni kwamba ata kama intaneti au umeme
utakatika ghafla usihofu kwani baadaye ukija
kuwasha faili lijajiendeleza kujishusha pale
lilipoishia mara ya mwisho.
Je jinsi gani ya Kutumia?
1. Shusha programu ya BitTorrent:
Programu za
BitTorrent ndo
zitakazokusaidia
katika kushusha
badala ya Kivinjari( au
‘Browser’ kwa
Kiingereza) kama
Firefox, Google
Chrome na zingine.
Programu maarafu za BitTorrent ni pamoja na
BitLord, BitComet , Vuze , BiTtornado, µTorrent ,
BitTorrent pamoja na QBitTorrent (Unaweza
ukabofya kwenye hayo majina na kwenda
kushusha). Nashauri Vuze, uTorrent, BitTorrent
au QBittorrent.
2. Tambua Sheria
Wengi hudhani kila kitu ni bure kwenye intaneti,
ila si hivyo. Kitu pekee kinachotulinda kwa kiasi
flani ni kwamba kwenye nchi nyingi
zinazoendelea kama Tanzania hakuna sheria na
kama zipo hazina nguvu sana katika masuala ya
haki miliki kwenye intaneti. Kwa hiyo kazi ni
kwako!
3. Jifunze Misamiati
Haya maneno ni ya kizungu ila ni muhimu
kuyajua kwani yatakusaidia kugundua kama faili
hilo litashuka upesi zaidi au litachukua muda
mrefu.
Leecher – Mtu anayelishusha(download)
ilo faili kwa wakati huo.
Seeder – Mtu anayepakia(uploading) faili
hilo kwa wakati huo. ‘Seeders’ wakiwa
wengi, ndio ‘Leechers’ au watu
wanaoshusha wataweza kulishusha kwa
mwendo mkali zaidi(high speed
download).
Tracker – Sio muhimu sana, ila ni taarifa
inayolihusu ‘torrent’ file hilo na usaidia
kupata taarifa juu ya Leechers na Seeders
la hilo faili kutoka mitandao mbalimbali.
Faili la Torrent (*.torrent) – Mara nyingi
hili ni faili dogo, ukishalishusha huwa
linaipa programu yako ya BitTorrent
kuhusu wakina nani wanahilo faili (kama
filamu, muziki, n.k) ili BitTorrent iweze
kulishusha kutoka kwao.
4. Tafuta Mafaili ya Torrent
Kwa
kuanzia
unaweza
kwenda www.kat.ph kwa vitu mbalimbali kama
filamu, muziki, tamthilia, programu n.k
5. Fungua hilo Faili la Torrent Ulilolishusha
kutoka Mitandao Hiyo.
Ukilibofya mara mbili (double click) au kulifungua
kwa namna nyingine yeyote litafunguliwa na
programu ya BitTorrent uliyokwenye kompyuta
yako. Inaweza kukuuliza unataka ku’save’ wapi
faili hilo litakaloshushwa chagua sehemu na acha
programu ifanye kazi yake.
NB: Kumbuka faili lenye ‘Seeders’ wengi na
‘Leechers’ wachache litashusha haraka zaidi.
6. Likimaliza kushusha kazi kwako…
By ITPhidel
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon