Umekwisha nunua memori kadi (SD Card) ya
GB 4, 8 n.k kisha muda wa kuitumia
unagundua ni nusu ya ujazo huo uliokua
umeandikwa kwenye kadi? Au data zinakuwa
zinapotea mara kwa mara…Basi ujue
umenunua SD Card feki.
Wengi huwa wanajikuta wanatumia pesa
zaidi wakijua wanapata memori kadi ya
ukubwa unaoonekana juu ya kadi hizo lakini
mwisho wa siku ni utapeli tuu.
Tunashukuru walioulizia juu ya jambo hili na
leo tutakufundisha njia kadhaa za kuzitambua
kama ni orijino au feki.
> KABLA YA KUNUNUA
Fahamu aina za Memori kadi (SD Card)
Kuna aina kuu tatu. Hapa cha muhimu kujua ni
kuzifahamu hizi alama zake, ukikuta memori
kadi imeandikwa ina ukubwa wa GB 8 na huku
ukiiangalia haina alama ya familia hiyo basi
utambue unanunua kimeo.
Aina Ujazo
SDSC or SD
Hizi zina ukubwa
wa hadi GB 4
SDHC
Ukubwa wa GB 4
– GB 32
SDXC
Ukubwa wa GB
64 – TB 2
Fahamu tofauti za muonekano wa logo na
majina yake, SDSC(SD), SDHC na SDXC…pia
kiasi cha ukubwa unaotegemewa kwa aina
hiyo ya memori kadi. Ukiona tu haviendani
ujue unanunua bomu. Kuna viwanda vingi
bubu vinavyotengeneza memori kadi na kuiga
majina ya makampuni makubwa lakini huwa
hizo logo wanaweka ovyo ovyo tuu.
Ukiangalia ujazo wa GB zake na alama zilizopo
utagundua kadi kadhaa katika hizi ni feki
Chunguza ata boksi kwa nje kabla ya kununua,
ukiangalia katika hili na ukilinganisha na
maelezo ya aina za memori kadi tulizokupa
basi utatambua ni feki
>USHANUNUA NA HAUNA UHAKIKA
Kama umeshainunua na unaona inasumbua
sumbua na unataka kujipa uhakikisho wa
ubora wake basi fuata njia hizi. Moja ya
kwenye kompyuta na nyingine ya kwenye
simu.
Kwenye Kompyuta
Kuhakikisha kwenye kompyuta kuna programu
kadhaa, leo nitazitaja mbili zaidi
zinazoaminika.
Kuna H2testw na FakeFlashTest. Kupitia
programu hizi utaweza kufahamu ujazo wa
ukweli ulio kwenye memori kadi au ata USB
Flash. Hakikisha unazi’test’ mpya mara baada
ya kununua ili kujihakikishia na hivyo kuwahi
kurudisha kama inawezekana. H2testw ndio
maarufu zaidi.
Muonekano wa h2testw
Download
> H2testw
> FakeFlashTest
Kwenye Simu
Pakua app moja inaitwa SD Insights.
App ya SD Insights ikitoa taarifa kuhusu kadi
iliyowekwa kwenye simu
Weka memori kadi yako kwenye simu na
fungua app ya SD Insights. Inatakiwa kukupa
taarifa zote muhimu kuhusu memori kadi yako.
Kama ni orijino au feki basi utapata kujua.
Utapata taarifa sahihi za ujazo (storage) wake,
kampuni iliyoitengeneza, tarehe ya
kutengenezwa na kama ni kimeo utafahamu
pia.
Download
> SD Insight
Je wewe ushawahi kuuziwa kimeo? Sasa
kupitia tuliyoyaeleza utakuweza kuepukana na
hadha hii.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon