Google My Activity; Fahamu na Kufuta vyote ufanyavyo vilivyounganishwa na Google

Amini usiamini Google wanafahamu mambo
mengi kuhusu wewe kuliko ata rafiki zako wa
karibu au ndugu zako. Unakubaliana na hili?
Google wanafahamu jana umefanya nini
kwenye simu yako ya Android, umetumia app
gani, umetembelea mtandao gani, umeenda
wapi na mambo mengine mbalimbali kuhusu
wewe.
Na sasa kukusaidia kwa urahisi kuweza
kufahamu yote wanayojua kuhusu wewe
Google wana huduma inayoitwa ‘My Activity’.
My Activity ni kitu gani hasa?
Ni orodha ya mambo yote ambayo mfumo wa
Google unafahamu kuhusu ulichofanya au
kutumia katika huduma zao zote – iwe
mtandao au kitu katika programu endeshaji
yao ya Android.
Pia utaweza hadi kutafuta kitu husika katika
orodha hiyo yenye data mbalimbali
zilizopangwa kuanzia mpya hadi za zamani.
Mitandao uliyotembelea
Video ulizotazama katika huduma za
Youtube
Apps na huduma ulizotumia kwenye
simu yako ya Android
Vitu ulivyotafuta katika Google Search
Jinsi ya Kufuta data zako zote
Kama umeona kitu ambacho hukitaki kiwe
kwenye data za Google basi unaweza kukifuta
kwa kubofya eneo la doti tatu – hizi zipo
pembeni kulia kwenye jambo unalotaka lifuta.
Je utaki Google kukufuatilia mtandaoni?
Google wamewezesha hili pia. Kama hautaki
Google kuweka kumbukumbu (record) ya
mambo yako basi unaweza weka ‘pause’
kupitia hapa -> https://
myaccount.google.com/activitycontrols
Ukiingia kwenye linki hiyo basi utaweza chuja
vitu ambavyo unataka kuwa na kumbukumbu
navyo na vile ambavyo hautaki kuweka
kumbukumbu katika akaunti yako ya Google. -
Search, Location, video za Youtube n.k.
Je kuna faida yeyote ya Google kuwa na data
hizi kuhusu wewe?
Wenyewe Google wamewahikikishia watumiaji
wake ya kwamba data hizo haziuzwi moja kwa
moja kwa mtu mwingine yeyote. Bali data hizo
hutumika na kompyuta zao katika kuhakikisha
wanakuletea matangazo ya maana kwako
kutokana na tabia zako za mtandaoni
(unafanya nini, unatembelea mitandao gani).
Pia kompyuta zao kuwa na data za kama vile
sehemu unazoenda (location) zinaweza
kusaidia katika kuhakikisha huduma zingine
kama vile za ramani (Google Maps) na ata za
utafutaji (Search) zinakuletea matoleo yaliyo
na maana zaidi kwako…kulingana na sehemu/
eneo/nchi uliyopo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post