Fahamu Matumizi ya camera

Unajua kama kamera ya simu janja yako
inaweza ikawa na matumizi lukuki ambayo
kwa namna moja au nyingine yanaweza
yakurahisisha maisha yako
1. Scan Nyaraka
Scan Nyaraka
Kamera ya simu janja yako pia inaweza ikawa
ina’scan’ nyaraka tofauti tofauti. Pata picha
unakuwa na ‘scanner’ ambayo ipo mfukoni
kwako. Unaweza uka ‘scan’ vitu kama vile
mikataba,risiti au kitu chochote kilichopo
katika karatasi na unataka ukifanye kiwe
kidigitali
Baada ya hapo unaweza ukaamua kutuma vitu
hivyo katika barua pepe au unaweza
ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG
Unataka ku’scan’ vitu?
Kwa iOS shusha Evernote
Kwa Android shusha Google Drive ndani yake
kuna kipengele cha ku’Scan’
2. Tumia Kamera Ya Simu Janja Yako Kama
Mkalimani Wako
Teknolojia inabadilisha dunia kwa kiasi
kikubwa sana miaka kadhaa iliyopita
ningebisha kata kata kama jambo hili
lingeweza kutokea. Hivi unajua unaweza
ukatumia kamera ya simu yako ili kutafsiri
lugha Fulani?
Kumbuka kuna maandhishi huwa yanaandikwa
na mara nyingi tunakuwa hatuyaelewi kwa
mfano ukiwa katika mgahawa ikaja menyu
yenye maandishi ya kigeni hapo ndipo huduma
hii utakapo ona ubora wake
Ukiwa na App ya Google Translate, ambayo
inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo
kwa kuweka kamera mbele ya maandishi
yaliyoandikwa na hapo App itafanya zoezi zima
la kutafsiri kwenda katika lugha unayotaka
3. Tumia Kama Kamera Ya Ulinzi
App Ya Silent Eye
Hivi ulishawahi kuwa na hamu ya kutumia
kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi?
Labda una kamzigo kako pale ndani na
unataka ukachunge. Ondoka shaka kuna App
maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo
yote. App hizi hutumia kamera ya simu janja ili
kugundua mwondoko wa aina yeyote (motion)
na kisha kukutaariffu kupitia barua pepe (e-
mail) yako
Kwa iOs shusha App ya Manything
Kwa Android shusha App ya Silent Eye
4. Fuatilia Barcodes Za UPC
Wakati mwingine wakati ukiwa unafanya
manunuzi ya vitu na ukawa huna uhakika
kama unanunua vitu imara achana na ku
Google, tumia kamera ya simu janja yako
kuweza kuichunguza bidhaa hiyo.
Zile App ambazo zinamsaidia mtu ku’scan
code’ za UPC zinampatia mtu taarifa za
bidhaa katika kiganja chake kabisa. Ukiachana
na taarifa kuhusiana na bidhaa bado utaweza
kufananisha bei tofauti tofauti ya bidhaa hizo
ili kujua kama umepewa bei nzuri au la
Kwa iOs shusha App ya Quick Scan
Kwa Android shusha App ya ShopSavvy
Barcode and QR Scanner
5. Shangaa Anga
App Ya SkyView
Hivi ushawahi kukaa usiku na ukawa
unashangaa anga na ukaanza kujiuliza
maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni
nyota au ni sayari zingine?
Sasa App ya Skyview kwa Android na iOs
itakupa majibu yote
App hii inatumia kamera ya simu yako katika
kukuonyesha jinsi anga ilivyo cha kufanya
hapa wewe elekeza kamera ya simu janja yako
katika anga.

Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
25 July 2016 at 04:26 delete

Naaam Mkuu naona
Nice by A.k.a ambakisye
Visit my blogspot
www.jobumwansasu.blogspot.com

Reply
avatar

Ads Inside Post