Simu janja ya bei rahisi zaidi duniani! Bei ni chini ya Tsh 8,000/= | Ksh 410

Kutana na Freedom 251 – Simu janja ya bei
rahisi zaidi duniani! Hakika kwa sasa hakuna
mshindani wa bei wa simu janja hii kutoka
kampuni moja huko nchini India.
Simu ya Freedom 251 iliyotambulishwa na
kuanza kuuzika kwa bei ya chini ya Tsh 8,000/
= | Ksh 410 ilisababisha hadi mtandao wa
kampuni iliyoitengeneza kushindwa kuhimili
watumiaji mamilioni walioutembelea mara
moja ili kuweza kujipatia simu hiyo.
Freedom 251 imetengenezwa na nani?
Simu janja hii ya Freedom 251 imetengenezwa
na kampuni mpya tuu isiyo na ata miaka miwili
katika biashara ya utengenezaji na uuzaji wa
simu – Ringing Bells iliyopo katika jimbo la
Uttar Pradesh huko nchini India. Bei yake ni
rupee 251 ambayo ni takribani dola 3.6 za
kimarekani.
Ina sifa gani?
Inakuja na toleo la Android 5.1 Lollipop
Kamera ya selfie ya megapixel 0.3 na
ile kuu ikiwa ni ya megapixel 3.2
Inakubali teknolojia za 2G na 3G
pamoja na WiFi
Ina betri la mAh 1450
Kioo (display) cha sentimita 10
Prosesa ya 1.3GHz quad-core
RAM ya GB 1 pamoja na diski uhifadhi
(storage) wa GB 8 – unaweza kutumia
memori kadi (SD Card) ya hadi GB 32
Inasemekana vitu muhimu (components)
katika simu hiyo wanavinunua kutoka
Taiwan. Wengi wanajiuliza kampuni hiyo
inawezaje kutengeneza faida kwa bei yao hii,
wengi wanaona simu hiyo inatakiwa iuzwe kwa
bei ya si chini ya dola 50 za Kimarekani.
Ili kuondoa gharama zaidi kampuni hiyo inauza
simu hiyo kupitia mtandao wao tuu. Simu hiyo
imetambulishwa Alhamisi wiki hii na tayari
imejipatia umaarufu duniani kote. Watu
waliopo nchini India wanaweza kununua simu
hiyo kupitia www.freedom251.com na simu
zitaanza kutumwa kuanzia mwezi wa sita.
Bado haijajulikana kama simu hiyo itaweza
kupatikana duniani kote, na ata kama ikiwa
hivyo basi bei itapanda kidogo kwa ajili ya
usafirishaji pamoja na faida za
wafanyabiashara – ila ata gharama hizo
zikiongezeka bado inaonekana simu janja hii
itaendelea kuwa ni ya bei ya chini sana.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post