DTEK50: BlackBerry New Phone

Kila unapofikiria mwisho wa simu za
BlackBerry umefikia ndio BlackBerry wanakuja
na kitu kipya cha kukuonesha bado wapo
katika biashara ya simu.
Fahamu kuhusu simu yao mpya, DTEK50,
simu inayosemekana inafaa kupewa sifa ya
kuwa simu salama zaidi dhidi ya udukuzi n.k.
Muonekano wa simu ya BlackBerry DTEK50
Simu hii mpya kutoka BlackBerry
inayofahamika kwa jina la DTEK50 itaingia
rasmi sokoni mwezi wa nane mwaka huu na
kwa kiwango cha bei cha takribani dola za
kimarekani 300 (t akribani Tsh Tsh 657,000/= |
Ksh 30,400/= )
Nini kipya?
Hii ndio simu ya kwanza ya Android iliyo ya
kugusa tuu(touchscreen) kutoka BlackBerry.
BlackBerry ndio wanasifika zaidi duniani kwa
kuwa na mifumo ya kiteknolojia salama zaidi
ya kiusalama wa data dhidi ya udukuzi katika
simu.
Na katika BlackBerry DTEK50 inaonekana
wanaona kutumia Android ambayo tayari ni
programu endeshaji maarufu zaidi
ukichanganya na teknolojia za BlackBerry za
usalama basi simu hii inaweza jipatia
umaarufu kwa watu na mashirika yanayojali
usalama wa data zao zaidi.
Simu hii ndiyo ilikuwa mwanzo inafahamika
kwa jina la siri la BlackBerry Neon
Sifa za kiundani
Kioo cha inchi 5.2 cha uwezo wa HD
wa 1080p
Prosesa ya Snapdragon 617
Kiasi cha RAM cha GB 3
Diski Uhifadhi (storage) GB 16 huku
ukiwa na uwezo wa kutumia memori
kadi
Betri lisilo la kutolewa la mAh 2,610
Kamera ya selfi ya MP 8 huku ile kuu
ikiwa ya MP 13.
Je itafanikiwa?
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya BlackBerry
ameshashusha kiasi cha mauzo ya simu kwa
mwaka ili biashara ya simu ionekane inaleta
maana kwao. Mwanzoni wakati
wanatambulisha simu janja ya BlackBerry Priv
alisema ili wao waweze kuendelea na biashara
ya utengenezaji simu basi ni lazima mauzo ya
simu zao yawe si chini ya simu milioni 5 kwa
mwaka…lakini sasa amebadilika na kusema
mauzo yawe si chini ya simu milioni 3 kwa
mwaka.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post