Nini maana ya hacking?

Nini maana ya hacking?

Kwenye ulimwengu wa cyber ,mtu anaeweza kugundua udhaifu kwenye  system na kuweza ku uharibu aidha kwa lengo baya au zuri mtu huyu huitwa mdukuzi(hacker)

Siku hizi watu wanadhani hacking ni kuhusu ku hack account za watu za facebook au kuhack websites.Ndio hivyo vyote ni sehemu ya field ya hacking lakini ni kijitone tu kwenye pande la barafu

Ili kuwa hacker unahitaji kwanza elimu ya msingi ya programming na interest na commitment ya kuwa hacker
Kila siku uwe tayari kujifunza na kujua kitu kipya.

Aina ya hackers

1.Script kiddie
Hawa ni watu wanaotumia tools,scripts,njia na programs zilizotengenezwa na hackers halisi.Hawa ni wale ambao hawajui vizuri system ilivyo lakini bado wanaweza kui haribu kwa kutumia njia ambazo teyar zipo,sio kwa kufata nini hackers wengine walikifanya bali kwa ku copy kila kitu.

2.White hat hackers
Jina jengine huitwa Penetration testers
Penetration testing ni kitendo cha kupima uwezekano wa uwepo wa upenyo kweny system
White hat hacker huwa na lengo zuri la kujua matatizo kweny system kwa lengo la kuiongezea ulinzi,mara nyingi huajiriwa na makampuni kwa lengo la kulinda system.

3.Black hat hackers
Hawa pia ni penetration testers lakini lengo lao huwa si kwa ajili ya ulinzi bali kuiharibu system ili aidha waibe taarifa mbalimbali au waharibu tu utendaji wake wa kawaida.Wanchokifanya ni kinyume na sheria za kimtandao.
Mfano Jonathan aliefungwa  jela miaka 16 baada yak u hack server za DTRA moja ya idara nyeti nchini Marekani
Jonathan pia ali hack server za NASA na kuiba software yenye thamani ya dola 1.7milion(zaidi ya bil 3 na nusu za kitanzania)

4.Grey hat hackers
Hawa ni hackers ambao hujibadilisha kutokana na hali iliyopo anaweza kuwa na lengo baya au zuri
Hackers wa kundi hili wengi hufanya hacking kama fun tu au kuikosoa sytem flani kwamba inamakosa au kuitangaza njia mpya ya hacking aliyoigundua.
Mfano mwaka 2013,Khali Shreateh ambae amekuwa akitolea kufanya reseach za ulinzi wa sytems za computer ali hack account ya facebook ya mgunduzi wa mtandao huo Mark Zuckerberg ili kum force arekebishe kosa aliloligundua ambayo ilimfanya aweze ku post kwenye ukurasa wa facebook wa mtu yoyote pasipo mtu huyo kupenda.Baada ya tukio hilo facebook walirekebisha tatizo hilo.

5.Hactivists
Hawa ni hackers wanaotumia ujuzi wao wa hacking kwa ajili ya kutetea uovu unaofanywa na serekali au chombo cha umma,kwa kutoa taarifa za siri zilizojificha,na mara nyingi huwa kwenye vikundi mfano Lulzsec
Mfano,kwenye uchaguzi wa Iran 2009 kundi la hackers lilitoa taarifa za siri zinazoelezea uovu wa serekali wakati wa uchaguzi

Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
Dave
AUTHOR
22 January 2021 at 14:56 delete

Hello everyone I want to introduce you guys to a group a private investigators who can help you with information you need in any situation in life and they are ready to follow you step by step until your case is cleared just contact +17078685071 and you will happily ever after
Premiumhackservices@gmail.com

Reply
avatar

Ads Inside Post