Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu

Kuna mengi sana unaweza ukawa ushasikia
sana kuhusu njia nzuri za kuchaji simu yako.
Pia utakuwa umeshasikia kuhusu ambayo
hutakiwi kufanya ukiwa unachaji simu.
Je yana ukweli wowote?
Leo tutakuelezea kwa uchache na kwa ukweli
mambo muhimu kuhusu kuchaji kwa simu na
usalama wa betri za simu wakati tukiwa
tunazichaji.
1. Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya
simu zinaua simu
Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili ila
ukweli ni kwamba usitumie chaja za ubora
mbovu. Chaja feki si chaja zote ambazo
hazitengenezwi na kampuni husika ya simu
bali ni chaja ambazo zipo chini ya kiwango. Na
hizi utazigundua kupitia bei zake, usikubali
kumiliki simu ya gharama halafu ukawa
mbahili katika kununua chaja za uhakika kisa
bei zake.
Cha kufanya soma kuhusu kiwango na ubora
wa chaja inayofaa kwenye simu yako kabla ya
kununua chaja isiyokuja na simu yako.
2. Usitumie simu yako wakati unaichaji
Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa
teknolojia inayotumika kwenye chaja na simu
ni salama kabisa. Cha kuhakikisha ni kwamba
unatumia chaja zilizo na kiwango/ubora wa
uhakika (original/quality). Kumbuka hapa
haimaanishi ni kwamba lazima iwe ni yenye
lebo/nembo ya kampuni husika bali hili ni
suala la kuwa ni chaja yenye ubora wa
uhakika.
3. Usizime simu yako kamwe!
Si kweli! Unashauliwa kuzima simu yake
angalau ata mara moja kwa wiki kwa angalau
lisaa. Simu kama vifaa vingine vyote vya
umeme ni muhimu kupata muda wa
kupumzishwa. Na jambo hili ndio linaboresha
zaidi uhai wa simu yako.
4. Kuchaji simu usiku kucha kutaiua/haribu
Usisikilize hii…si kweli! labda kama unatumia
simu iliyotengenezwa miaka ya 1980 :-).
Teknolojia imekua sana, fahamu ya kwamba
simu zote za siku hizi zitaacha kutumia
umeme pale simu yako itakapochaji hadi
asilimia 100! Itaacha kuchaji! Hakuna
madhara! Ila hii haimaanisha ndio uiache kwa
zaidi ya masaa 15! na pia kuhakikisha
unaichaji sehemu inayopata hewa
5. Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au
imeisha ndio uchaji
Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji mara
kwa mara ndio kunasaidia zaidi kuongeza
maisha ya betri yako. Kumbuka kuchaji mara
kwa mara si kila baada ya dakika 5, bali ni
kwamba usisubiri chaji iwe chini ndio uchaji,
na si lazima ukiweka kwenye chaji usiitoe hadi
imejaa.
6. Kuna aina kuu mbili za mabetri yanatumika
kwa sasa
Kuna mabetri yanayotumia teknolojia
ya Lithium-Ion (Li-ion) na Lithium-Ion-Polymer
(Li-ion polymer/Lithium Polymer). Kuna
teknolojia nyingi zilizokuwepo zamani ila kwa
sasa hizi ndio zinazotumika zaidi. Na
zinatumika kutokana na ubora wake. Lithium-
Ion (Li-ion) zinatumika zaidi katika simu nyingi
zaidi wakati mabetri ya Lithium-Ion-Polymer
yanatumika zaidi katika laptop na baadhi ya
simu pia. Lithium-Ion-Polymer ndio teknolojia
bora zaidi na salama zaid, lithium-Ion ni
salama pia kwa kiwango kikubwa sana ila
lithium-ion-polymer ni zenye ubora zaidi na hii
inaweza kuwa ni sababu kubwa zinatumika
kwenye laptop nyingi tayari. Teknolojia hizi
zimefanya ulipukaji ovyo wa mabetri ya simu
kuwa mgumu sana kuliko unavyofikiri.

Previous
Next Post »

2 comments

Write comments

Ads Inside Post