Jinsi Ya Kufufua Meseji Zilizofutika Katika Android Na iOS!

Unaweza ukawa wewe ni mmoja kati ya watu waliofuta meseji zao za muhimu kwa bahati mbaya. Ndio hii inatokea kwa wengi, kikubwa watu wanachofanyaga ni kujilaumu wenyewe. Lakini vipi kama kungekuwa na njia nyingine ya kufufa meseji hizo?
Unaweza ukawa umefuta meseji ambayo ina taarifa za muhimu kama vile malipo na kumbukumbu namba. Kaa mkao wa kula TeknoKona inakuletea maujanja ya kuzifufua meseji hizo.
Jinsi Ya Kufufua Kwa Vifaa Vya Android!
Najua watumiaji wa Android ni wengi sana. Ukiachana na hilo njia hii itakufanya uwezo kufufua meseji zako bila shaka kwa kufata njia hizi
1. Shusha software ya ufufuaji Coolmuster sms+contacts katika kompyuta yako
2. Sasa inakubidi uiunganishe simu yako na kompyuta kwa kutumia USB ili kuanza kufufua meseji zako.
3. Sasa anza ku ‘scan’ kifaa chako cha Android kwa kutumia programu hii
4. Ukishamaliza kufanya hayo hapo utakuwa na uwezo wa kuweza kuona meseji zako zote ambazo zimefutwa mbali na hayo unaweza ukazihifadhi katika simu yako ya Android.
5. Ukishachagua meseji ambayo unataka kuifufua chagua ‘Recover’ ili kuziweka katika simu yako.
Mpaka hapo hautahofia tena kuhusu meseji zako zilizofutika au ambazo utazifuta kwa bahati mbaya
Coolmuster sms+contacts
Jinsi Ya Kufufua Kwa Vifaa Vya iOS!
Hakuna tofauti kubwa sana ya kufufa meseji zako kwenye vifaa vya iOS (kama iPhone) ukilinganisha na njia ile ya Android. iPhone inatoa huduma nyingi tuu ya njia ambazo unaweza ukazitumia kufufua meseji zako. Hapa ntakupa njia rahisi ambazo unaweza ukatumia
Fufua Meseji Katika Matoleo Ya iPhone 4s Na Kuendelea
1. Shusha software ya kufufua meseji zako ( Coolmuster iPhone Data Recovery) na ipakue katika kompyuta yako
2. Ukishamaliza kuipakua katika kompyuta yako. Unganisha iPhone yako katika kompyuta kisha anzisha programu hiyo
3. Ukishafunguka ‘click’ eneo la ‘Recover From iOS Device’ baada ya hapo utapata ujumbe unaokuambia kwamba kifaa chako cha iOs kimeunganishwa
4. Anza ku ‘scan’ ili kuendelea. Baada ya zoezi hili kuisha itaonyesha meseji zote ambazo zilifutika. Weka tiki katika meseji ambayo unataka kuifufua na kisha chagua ‘Recover’
5. Kama unataka kuhifadhi meseji hizo katika kifaa chako chagua ‘Recover To Devicce’
Coolmuster iPhone Data Recovery
Mpaka hapo utakuwa huna wasi wasi kabisa wa kupata meseji zako ambazo zimefutika. Kwa watumiaji wa iPhone 4 kurudi nyuma mpaka iPhone 2G tutawatafutia ufumbuzi maana wanaweza wakatumia njia hii alafu kwa bahati mbaya ikagoma

Previous
Next Post »

Ads Inside Post