Google Chrome yaachana na XP,VISTA na OS X za zamani

Google wametoa toleo jipya la browser yao ya Chrome, pamoja na maboresho ya browser hii Google wameondoa msaada (support) wa toleo hilo kwa kompyuta zinazotumia matoleo ya zamani ya OS za XP, VISTA na OS X.
Google wanakuwa wametiza ahadi yao waliyoitoa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita ya kwamba wangeachana na huduma hii mwisho wa mwaka 2015, mwaka jana mwishoni waliongeza muda wa ku support OS hizo za zamani hadi mwezi 4 2015.
Google chrome wanaachana na OS za XP Vista na OS X za zamani kwa kuwa hazifikii viwango vya chini vinavyohitajika na kisakuzi hicho cha Google, hii ina madhara katika ubora wa huduma ambao Google chrome itakuwa inatoa katika kompyuta ambazo zinatumia.
Sasa Google wataelekeza nguvu katika kutengeneza Chrome ambayo itafanya kazi kwa kiwango cha juu katika kompyuta zenye OS za kisasa.
Kuanzia sasa kompyuta zote ambazo zinaendeshwa na XP Vista ama OS x matoleo ya zamani hazita pokea update yeyote, hazitakuwa na uwezo wa kupokea huduma za kimsaada kutoka Google. Watumiaji ambao bado wanatumia OS hizi wanashauliwa kuhama na kutumia OS za karibuni zaidi ili kuendelea kufaidi huduma za Google Chrome.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post