Makosa ya kimitandao

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA, limemkamata na kumfikisha mahakamani mtu mmoja anayefahamika kwa majina ya Issack Habakuki Emily Mkazi wa Olasiti Jijini Arusha kwa kosa la kutumia lugha chafu na ya kejeli dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.Akisoma Mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile,Wakili wa Serikali Gaudensia Massanja amedai kuwa mtuhumiwa huyo anakabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi Emily alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Rais MAGUFULI.
Alidai mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosomeka “hizi ni siasa za maigizo,halafu mnamfananisha huyu bwege na nyerere,wapi buana”
Kwa upande wake mtuhumiwa Emily akaiomba Mahakama hiyo kumpa dhamana kwani ni haki yake hoja ambayo ilipingwa na wakili wa Serikali Massanja aliyedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo kumpatia dhamana mtuhumiwa kunaweza kuharibu upepelezi.
Akitoa uamuzi mdogo wa hoja za pande mbili Mahakamani hapo,Hakimu Mkazi RWIZILE alisema uamuzi kamili wa dhamana ya mtuhumiwa huyo utatolewa April 18 Mwaka huu.
Awali wakizungumza na wanahabari juu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo pamoja naye Mwanasheria wa Mamlaka ya mawasiliano Nchini Johanes Kalungula wamedai mtuhumiwa alikamatwa katika hoteli ya Annex Jijini humo

Previous
Next Post »

Ads Inside Post