Instagram – sasa waleta Video channel

Instagram wameleta Video channel ambacho ni kitu kipya katika app yake na pia imefanyia mabadiliko ukurasa wake wa Explore ambao kwa sasa itakuwa inakuwa na video ambazo zimeandaliwa kutokana na vitu ambavyo Instagram inahisi wewe ungependa kuviona.
Instagram imefanya mabadiliko haya ambayo wengi wanayaona ni katika jitihada za kuhakikisha kwamba mtandao mpya wa Snapchat hauitoi instagram katika nafais yake iliyopo sasa.
Mabadiliko haya yameukumba ukurasa wa Explore na kuleta muonekano mpya ambao utatumia algorithim kujua ni video gani unapendelea kuangalia na kuziweka hapo ili uweze kuziona kwa urahisi.
Pia mabadiliko haya yanaleta huduma ya Video channel ambayo haikuwepo hapo mwanzo ambayo inakupa mkusanyiko wa video ambazo zina maudhui ambayo yanafanana. Kwa huduma hizi instagram wameendelea kuonesha kwamba wanajaribu kuwakamata wateja wengi kwa kuelewa kwamba watumiaji wengi sikuhizi wanapendelea video zaidi.
Kwa sasa sisi ambao tulikuwa hatufurahii video za instagram kucheza na kuendelea kujirudia tumepata mkombozi, ukiwa unaangalia video katika ukurasa wa Explore sasa video hazitacheza katika namna ya kujirudia bali kila video itacheza mara moja na kisha video inayofata itacheza,
Mabadiliko haya yameanza kwa watumiaji walio Marekani kwa upande wa iOS pamoja na Android na yataanza kusambaa taratibu

Previous
Next Post »

Ads Inside Post