Hiki ndicho kilichofikiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Kahama.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu
uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka jana
iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge
kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Kahama mjini
Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea wa CCM
Mh.Jumanne Kishimba imeendelea leo katika
mahakama ya wilaya ya Kahama.
Kesi hiyo amnbayo iliendelea kuunguruma leo
majira ya saa tano kamili huku wananchi
waliofika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo
wa kesi hiyo wakiilalamikia mahakama kutoweka
vipaza sauti hali inayosababisha idadi kubwa ya
wananchi waliofika kusikiliza kesi hiyo kushindwa
kuelewa nini kinaendelea.
Aidha baada ya jaji Moses Mzuna kusikiliza hoja
za kila upande na kuridhika na maelezo aliagiza
pande zote mbili kuleta mashahidi wao ili
waanze kutoa ushahidi na kuahirisha kesi hadi
kesho siku ya jumatano tar.02/03 ambapo kesi
itaendelea.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post