Bei ya nishati ya mafuta imeendelea kushuka
baada ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za
nishati na maji EWURA kutangaza bei kikomo
huku baadhi ya wananchi wakitaka bei za bidhaa
nazo zishuke.
Akitangaza bei elekezi jijini Dar es Salaam
mkurugenzi mkuu wa EWURA Bw.Felix
Ngamlagosi amewataka wateja wa nishati ya
mafuta kudai risiti pindi wanapopewa huduma
hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi
wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za
kiganjani.
Baadhi ya wananchi wameeleza kushangazwa na
kitendo cha nishati hiyo kushuka mara kadhaa
lakini bei za bidhaa kuendelea kupanda na
kuitaka serikali kuunda tume ya bei huku wauzaji
wa nishati hiyo wakielezea changamoto
wanachokabiliana nazo katika kutoa risiti kwa
wateja.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon