Mbowe aitwa haraka mbeya kunusuru chama baada ya kuibuka Mgogoro.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha
demokrasia na maendeleo, CHADEMA,wilaya ya
mbeya mjini wamemtaka mwenyekiti wa chama
hicho taifa,Fremman Mbowe kwenda haraka jijini
Mbeya kutatua mgogoro wa kiuongozi
unaoendelea ndani ya chama kabla haujaleta
madhara makubwa na kusababisha chama hicho
kupoteza imani kwa wananchi.
Tamko la wajumbe hao wa mkutano mkuu wa
Chadema wilaya ya Mbeya mjini linatokana na
kikao cha ambacho kilifanyika hivi karibuni chini
ya usimamizi wa makamu mwenyekiti wa
Chadema taifa upande wa Zanzibar,Mohamed
Issa Mohamed kilichoamua kuvunja kamati ya
utendaji ya chama hicho wilaya ya Mbeya mjini
na kuweka uongozi wa muda, jambo ambalo
linapingwa vikali na wajumbe wa mkutano mkuu
wa chama hicho.
Kutokana na hatua hiyo baadhi ya wajumbe wa
mkutano huo wakadai kuwa wao hawautambui
uongozi wa muda uliowekwa na badala yake
wataendelea kuwatambua viongozi
waliowachagua kikatiba.
Akitoa tamko la pamoja, katibu wa mkutano
huo,Hezron Edwin Mwaisengela amesema kuwa
wajumbe wanamtaka mwenyekiti wa chama taifa
kufika mbeya haraka ili kutatua mgogoro huo
kwa maslahi mapana ya chama.
› Mbowe aitwa haraka mbeya kunusuru
chama baada ya kuibuka Mgogoro.
1

Previous
Next Post »

Ads Inside Post