Wanawake zaidi ya 450 nchini hupoteza maisha
wakati wa kujifungua kati ya vizazi hai laki moja
kwa mwaka vinavyosababishwa na huduma
mbovu za afya ya uzazi, vifaatiba, uhaba wa
wakunga na wauguzi katika vituo vya afya na
hospitalini pamoja na ubovu wa miundombinu ya
barabara.
Akitoa takwimu hizo kwenye mkutano uliohusisha
wakunga na wauguzi wa mikoa na wilaya hapa
nchini meneja miradi Amref Tanzania Dokta
Piusi Chaya amesema kufuatia vifo hivyo na
changamoto ya uhaba wa wauguzi shirika hilo
limejetolea kusomesha wauguzi 254 kwa ngazi ya
cheti huku wengine 80 wamehitimu masomo yao
na tayari wamerejea katika vituo vyao vya kazi.
Kwa upande wao baadhi ya wakunga na wauguzi
wakuu wa mikoa wamesema wanakabiliwa na
changamoto nyingi zinazokwamisha utenda na
kuwahudumia wanawake wajawazito na kuokoa
maisha yao wakati wa kujifungua na hapa
wanaeleza.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon