Bariadi leo Zaidi ya nyumba 30 zabomolewa, Bariadi kupisha ujenzi wa barabara.

Zaidi ya nyumba 30 zimebomolewa mjini Bariadi
chini ya usimamizi wa wakala wa barabara na
jeshi la polisi, huku zoezi hilo likisimama kwa
muda wa dakika 20 kufuatia mabishano makali
na baadhi ya mmiliki wa nyumba akidai kutopewa
notisi, mwingine kukataa kutoka ndani ya nyumba
na kulazimika kutolewa kwa nguvu na askari
polisi.
Zoezi hilo ambalo limeanza majira ya saa kumi
na mbili asubuhi huku likikumbana na vikwazo
vya malumbano na baadhi ya wamiliki kugoma
kubolewa nyumba zao kwa madai ya kutopewa
notisi, huku nyumba hizo zikiwa na alama za X
na baada ya dakika kadhaa zoezi hilo likaendela.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa
Bariadi, Athuman Hamisi amekiri kuwa watu wote
waliokuwa wanatakiwa kubomoa nyumba hizo
walipokea barua za kubomoa ndani ya siku 30,
huku baadhi ya umati uliofurika kushuhudia
ukiunga mkono kufanyika zoezi hilo ambalo liko
kisheria.
Akizungumzia zoezi hilo meneja wa Tanroad
mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent amesema
kuwa wametekeleza zoezi hilo kwa watu
waliokaidi kubomoa ili kuweza kupisha shughuli
za ukamilishaji wa ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami kutoka Lamadi hadi mjini
Bariadi unajengwa na kampuni ya kichina ya
CCCC.
› Zaidi ya nyumba 30 zabomolewa, Bariadi
kupisha ujenzi wa barabara.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post