Mke wa Rais Janeth Magufuli akimjulia hali Sheikh Mkuu wa Tanzania katika Hospitali ya Muhimbili.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mama Janeth Magufuli amemtembelea
na kumjulia hali Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Abubakary Zubeiry aliyelazwa katika Taasisi ya
Moyo ya Dakta Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mama Janeth Magufuli amewaomba watanzania
wazidi kumuombea mufti Zubeiry apone haraka ili
aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya
Dakta Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi
amesema mufti Zubeiry kwa sasa anaendelea
vizuri.
Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewatoa
hofu waumini wa dini ya kiislam nchini na
watanzania kwa ujumla kuwa Mufti Zubeiry afya
yake kwa sasa inazidi kuimarika.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post