Zaidi ya nyumba 100 katika mtaa wa Bulyehele
wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza zimekutwa
zikitumia umeme kwa njia ya wizi, baada ya
mafundi wa shirika la ugavi wa umeme
(Tanesco) mkoani humo kufanya ukaguzi wa
kushtukiza na kukuta baadhi ya nyaya zilizokuwa
zinatumika kusambaza umeme huo kwa
wananchi zikiwa zimechimbiwa ardhini.
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Bulyehele Peter
Nkomba anasema sababu kubwa ya baadhi ya
wananchi kujihusisha na wizi wa umeme ni
kutokana na urasimu unaosababishwa na baadhi
ya watendaji wa Tanesco, huku Bi. Siwema
Kenedy mkazi wa mtaa huo akieleza wasiwasi
wake juu ya hatari ya kuchimbia nyaya za
umeme chini ya ardhi hasa kipindi hiki cha mvua
zinazoendelea kunyesha.
John Chilale ni afisa usalama wa Tanesco mkoa
wa Mwanza, anatoa angalizo kwa wananchi
kuacha kujiunganishia umeme kinyemela, kwani
hali hiyo inachangia kupoteza mapato ya shirika
na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili
kuwabaini baadhi ya watu wanaolihujumu shirika
hilo, ambapo afisa wa kitengo cha kudhibiti
mapato wa Tanesco mkoa wa Mwanza Mhandisi
King Fokanya amesema wamebaini kuwa umeme
huo umekuwa ukisambazwa kwenye nyumba hizo
zaidi ya 100 na wateja halali watatu walio na
mita zinazotambulika na shirika hilo.
Tangu kuanza kwa operesheni inayojulikana kama
‘kamata wezi wa umeme (kaweu) mwezi
Desemba mwaka jana, zaidi ya watu 18 mkoani
Mwanza wamekamatwa na shirika hilo kwa
tuhuma za kujiunganishia umeme bila kufuata
taratibu za Tanesco na kulisababishia shirika hilo
hasara ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon