Jeshi la polisi kitengo cha majini kimekamata mafuta ya wizi katika bandari ya Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi kitengo cha majini kimekamata
tani zipatazo 20 za mafuta ya Dizeli yaliyokuwa
katika Jahazi lililokuwa kando ya bandari ya Dar
es Salaam likijiandaa kwa safari ya kwenda
Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo hicho cha polisi cha wanamaji
Bwana Mboje John Kanga amesema watu
watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na
uchunguzi zaidi unaendelea.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post