Sakata la kupanda bei ya sukari limechukua sura
mpya baada ya umoja wazalishaji wa Sukari
kudai kuwa kuna njama za baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa ambao mianya yao ya
uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi imezibwa
hivyo wameanza kuhujumu sukari ya ndani.
Mwenyekiti wa umoja wa wazalishaji hao wa
sukari balozi Ami Mpungwe amesema wana
uhakika njama za wafanyabiashara hao
hazitafanikiwa kwani bei halisi ya Sukari ambayo
inapaswa kuuzwa kwa rejareja haitakiwi kuzidi
elfu mbili kwa kilo moja.
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari
Abdul Mwankemwa amesema kuna
wafanyabiashara ambao wamehodhi sukari katika
maghala kwa lengo la kuifanya iwe adimu na
hivyo bei yake kupanda.
Kuhusiana na kwanini bei ya sukari kutoka nje ya
nchi kuuzwa kwa bei nafuu kuliko ile
inayozalishwa ndani ya nchi mmoja wa
wazalishaji hao wa Sukari Seif Ali Seif kutoka
kiwanda cha Sukari Kagera anaeleza.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon