Jeshi la polisi lakamata kontena la ving’amuzi feki visiwani Zanzibar.

Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kukamata
kontena liloingizwa Zanzibar likiwa na vingamuzi
feki zaidi ya 1000 kutoka China ambavyo vilikuwa
viingizwe sokoni.
Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa upelelezi na
makosa ya jinai Zanzibar kamishna msaidizi
Salum Msangi amesema polisi kwa kushirikiana
na polisi wa kimataifa Interpol na kampuni ya
kimatiafa ya ushauri wa kulinda alama za
biashara kontena hilo limenaswa bandarini
Zanzibar na kukutwa na vingamuzi hivyo
vilivyokuwa na lebo za Singsung na Blackstone
ambavyo vyote vilikuwa ni feki na polisi
inaendelea kuwasilaina na makampuni husika.
DCI Salum Msangi pia katika mkutano huo
ametahadharisha jamii kuwa jeshi hilo litaanza
kuwachukulia hatua bahadhi ya watu na
mitandao ambayo imekuwa ikitukana viongozi na
kutoa lugha za matusi na polisi imeanza
kuchukua hatua hizo.
Hatua hizo za polisi zimekuja wakati
pamekuwapo na malalamiko ya Zanzibar
kutumika kwa kuingiza vyakula na vifaa vya
umeme ambavyo ni feki na pia bandari na uwanja
wa ndege wa Zanzibar kutumika kusafirisha
madawa ya kulevya ambapo jehsi hilo pia
limefanikiwa kuwakmata watu wawili akiwemo
raia wa Ethiopia waliongiza madawa ya aina ya
Mirungi kwa njia ya kukausha.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post