Wauguzi kwenye zahanati tatu zilizopo katika
kata ya Harugu wilayani Mbozi wanalazimika
kutumia TOCHI na simu za mkononi kwa ajili ya
kupata mwanga wa kuwasaidia kuwahudumia
wajawazito nyakati za usiku kutokana na
kutokuwa na nishati ya umeme, hali ambayo
wakati mwingine huchangia kutokea vifo vya
wajawazito.
ITV imetembelea zahanati za kata hiyo ya
Harungu ambazo ni Halambo, Hampangala na
Shazya na kukutana na wauguzi wanaotoa
huduma kwenye maeneo hayo ambao wamedai
kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni
ukosefu wa nishati ya umeme hali inayowalazimu
kuwahudumia wagonjwa hasa wajawazito kwa
kutumia tochi na simu za viganjani.
Kwa upande wa wananchi hasa wanawake
wamelalamikia upatikanaji wa dawa na tabia ya
wauguzi hao kuwauzia kadi kwa ajili ya kuwekea
kumbukumbu wakati wanapohudhuria kliniki.
Diwani wa kata ya Harungu,Maarifa Mwashitete
amesema amekwishatembelea zahanati hizo na
kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo hiyo ya
umeme na tayari ameanza kuchukua hatua za
kupeleka Solar na mabomba ya sindano kwa ajili
ya kupunguza kero zinazowakabili wananchi
wanaofika kwenye zahanati hizo kupata huduma.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon