Huu Ndio Uamuzi wa Tip Top Kuhusu Dogo Janja Baada ya Kulalamika Kuwa Wanambania

Baada ya kuvuja kwa sauti ya Dogo Janja
akilalamika (kwa demu) kuhusu uongozi
wake wa Tip Top connection kumbania,
Madee ametoa uamuzi walioamua
kuuchukua.
Madee alianza kwa kusema kuwa hakuwa na
taarifa yoyote juu ya malalamiko yoyote ya
Dogo Janja kubaniwa mpaka alipokutana
nayo kwenye audio hiyo iliyosambaa
mitandaoni, na kuongeza kuwa siku moja
kabla ya audio hiyo kuvuja alikuwa na Dogo
Janja wakimalizia video ya wimbo wake
mpya na hakujua kama kuna tatizo lolote.
Hii ndio kauli ya Madee kuhusu uamuzi wa
Tip Top juu ya Janjaro;
“Mimi nabaki kwenye maamuzi ambayo
tumeshaongea na Tale, kwamba hatuwezi
kutoa maamuzi ambayo wao wanadhania
yatakuwa ni ya kumkandamiza moja kwa
moja Dogo Janja, kwa sababu sawa,
mwanaume kama mwanaume unapoamua
kutongoza unatumia mbinu zako nyingine
nyingi tu, yeye ndio ile mbinu ambayo aliona
anaweza.” alisema Madee.
“Lakini kama kazi zake sisi tumezifanya na
tumeshafanya kila kitu video tayari kwahiyo
sidhani kama kweli yale maneno yametoka
moja kwa moja kwenye moyo wake kina
Madee wananibania wakati tayari kazi zake
zimeshafanywa na ratiba yake
imeshafanywa, nachoamini mimi ni kwamba
alikuwa anataka kumuwin tu Yule
mwanamke, lakini kikubwa ambacho
amehaaribui ni matusi pamoja na kutoa siri
ambazo yeye anaona ni sawa kuzisema.”
Alieleza Madee.
Licha ya Janjaro kufanya hayo, Madee
amesema kuwa hawatasitisha kutoa kazi
zake ambazo tayari zilikuwa kwenye ratiba
ya kutoka.
“Ratiba lazima ziendelee kwasababu tayari
tumeshapata hasara tumeshatoa hela za
kufanya audio , video ratiba itaendelea lakini
lazima Dogo Janja atakuwa chini ya
adhabu.” alisema Mdee

Previous
Next Post »

Ads Inside Post