Diwani wa kata ya Kambarage iliyoko mjini
Shinyanga Mh.Ramadhani Mwendapole
amelazimika kuingilia kati na kuzuia vurugu kati
ya wananzengo na familia ya Bw.Kalistus
Shirima kugombea mwili wa marehemu Emiliani
Peter Kulwa miaka 26 aliyefariki dunia katika
mazingira ya kutatanisha ambapo familia hiyo
ilizuia mwili wa marehemu usiagwe kwa heshima
za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda
kuzikwa nyumbani kwao moshi Kilimanjaro.
Wakizungumza kwa masikitiko wanaumoja wa
kusaidiana katika shida na raha maarufu kama
wananzengo wamedai kuwa wakati marehemu
akiwa mgonjwa ndugu zake walikuwa wakiwazuia
watu wasimujulie hali mgonjwa huku wakidai
kuwa kifo cha Emiliani Kulwa kimesababishwa na
uzembe wa ndugu zake kwakuwa hata alipofariki
hakuna mtu yeyote aliyekuwa karibu naye na
ndugu hao walikuwa katika biashara zao hadi
alipotokea msamaria mwema ndipo akagundua
kuwa mgonjwa ameshapoteza maisha.
Aidha wakati diwani wa kata ya kambarage
Mh.Ramadhani Mwendapole alipoingilia kati na
kutuliza ghasia hizo ndipo wanafamilia
wakaamua mwili wa marehemu Emiliani Peter
Kulwa uletwe mahali hapo ili uagwe kwa heshima
za mwisho tayari kwa kusafirishwa kuelekea
moshi kwa mazishi huku mwenyekiti wa mtaa wa
Kambarage Bi.Fatuma Juma akitangaza faini ya
shilingi laki tano kwa familia ya marehemu kwa
kosa la kuzuia marafiki na wanazengo
kumhudumia mgonjwa na kufanya uzembe
unaodhaniwa kusababisha kifo cha marehemu
emiliani kulwa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon