Watu watano wa familia moja wakiwemo watoto
watatu katika mtaa wa Sume kata ya
Mwembesongo manispaa ya Morogoro
wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi
kuangukiwa na ukuta wa uzio wa kituo cha
mafuta cha total usiku wakiwa wamelala.
ITV imefika katika eneo hilo na kushuhudia
nyumba hiyo ikiwa imebomoka kabisa upande wa
nyuma ambapo majeruhi wa tukio hilo wameeleza
jinsi lilivyotokea huku wanafamilia wamelalamikia
kulala nje kwa zaidi ya siku tatu na hawajui
hatima yao kutokana na mmiliki wa kituo hichi
kushindwa kuwasaidia na kwamba kabla ya ukuta
huo kuanguka walitoa tarifa lakini hazikufaniwa
kazi.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa
Sume Hamis Totoro amesema tukio hilo
limetokea majira ya usiku ambapo majeruhi
waliwahishwa hospitali ya rufaa ya mkoa
Morogoro pamoja na hali zao kuendelea vizuri
lakini mmoja wao ambaye ni mzee
amehamishiwa katika hospitali ya Agakan jijini
Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Kufuatia tukio hilo ITV imemtafuta mmiliki wa
kituo hicho cha mafuta cha Total bila mafanikio
baada ya simu yake kuita bila kupokelewa
ingawa pia wafanyakazi wa kituo hicho
wameshindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi
wa habari huku wakiwazuiya kupigapicha kituo
hicho.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon