Mwekezaji alalamikia mkuu wa wilaya ya Kilosa kudharau hati ya hukumu ya mahakama kuu ya ardhi.

Mwekezaji wa shamba la kampuni ya Mees
Estate katika kijiji cha Mbigiri wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro amelalamikia mkuu wa wilaya
hiyo Bwana John Henjewele kuwaruhusu
wananchi kuingia kwenye shamba lake lenye
ukubwa wa hekari 1500 huku akitambua
mahakama kuu tayari imetoa hukumu juu ya kesi
ya shamba hilo na imempa haki mwekezaji huyo.
Akizungumza na ITV meneja wa shamba hilo
Bwana Patric Anthoni amessema anashangazwa
na hatua ya mkuu wa wilaya ya Kilosa kushindwa
kuheshimu maamuzi ya mahaka kwa
kuwaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za
kilimo katika shamba la kampuni jambo ambalo
linaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Nao wasimamizi wa shamba wamesema
walivamiwa na kundi la wananchi wakidai
kuagizwa na mkuu wa wilaya ya Kilosa
kuhakikisha wanalinda shamba hilo ambapo
kufuatia uvamizi huo jeshi la polisi kikosi cha
kutuliza ghasia kimefika katika shamba la
mwekezaji huyo na kukuta wananchi
wamekwisha tawanyika na hivyo kuimarisha
ulinzi katika shamba hilo.
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya
ya Kilosa Bwana John Henjewele amesema
muwekezaji huyo kama ana malalamiko ya
msingi afuate ngazi za kisheria ili malalamiko
yake yaweze kufanyiwa kazi na sio kulalamika
kwenye vyombo vya habari.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post