Zaidi ya watu mianne wa kijiji cha Themiyasimba
wilaya ya Arumeru wameandamana hadi kwenye
shamba la mwekezaji wakitaka kugawana
sehemu ya shamba ilo kwa madai mwekezaji
amepewa shamba la hekari elfu tatu lakini
ameshindwa kuliendeleza na kuanza kuuuza kwa
wawekezaji kutoka nje huku wananchi wakikosa
ardhi ya kuweka huduma muhimu za kijamii hali
iliyowalazimu viongozi wa kijiji na kata kuingilia
kati kisha wananchi wakatoa wiki moja la sivyo
watafanya maamuzi magumu.
ITV ilifika katika kijiji cha Themiyasimba na
kushudia umati mkubwa wa wananchi waliyo
zungumza kwa jazba wakisema wamefikia hatua
hiyo baada ya kuteseka kwa muda mrefu bila
huduma za kijamii kama shule zahanati na kituo
cha polisi huku wakizungukwa na mashamba
makubwa yasiyo endelezwa na kuuzwa kwa
wawekezaji kutoka nje ambao wengine uyauza
tena na kuwakata wananchi wanunue hekari moja
kwa shilingi milioni mbili huku wakitambua
kwamba hawana uwezo huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Themiyasimba Emanuel
Wiliam alitumia muda mrefu kuwaomba wananchi
kuacha kugawana shamba ilo kwakuwa ni
kinyume cha sheria na kuwataka kuwa nasubira
wakati wakifanya mawasiliano na uongozi wa juu.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bwawani
Lazaro Lukumay amesema kumekuwa na tabia
ya wawekezaji kupewa mashamba makubwa na
kushindwa kuyaendeleza kisha kuyauza na
kuwakodisha wananchi kwa bei ya juu hivyo
ameitaka serikali kuangalia upya umiliki wake ili
kuepusha migogoro isiyo na tija.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon