liyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa
mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba
ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa
amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata
suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar
kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio
machi 20 mwaka huu.
Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini
kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa
kikao chake na wazee kutoka chama cha
Chadema ambapo amesema anaunga mkono
uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku
akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza
mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya
kisiasa Zanzibar ikabadilika.
Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na
uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika
kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia
ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa
kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa
ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania
waliojitokeza kupiga kura mapema 25 ,huku pia
akiigusia katiba ya Tanzania.
Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa
na mzee Enec Ngombare wamempongeza Mh.
Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya
uchaguzi ambapo pia wamemhakikishia kuwa
wako pamoja nae katika safari ya kuelekea
mwaka 2020.
Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada
wa siku nyingi Kingune Ngombare Mwiru, Mh
Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania
kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha
wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi
hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za
kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon