Wanasheria na mawakili wanaoendesha kazi zao kinyume cha sheria waonywa Kigoma.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu
Issa Machibya amewaonya wanasheria na
mawakili wanaoendesha kazi zao kinyume cha
sheria na kusababisha kuongezeka kwa migogoro
katika jamii.
Machibya ametoa onyo hilo wakati wa
maadhimisho ya siku ya sharia nchini ambapo
amesema, wapo watu wanaojifanya wanasheria
wa kujitegemea wamekuwa wakipita maeneo
mbalimbali katika mkoa wa Kigoma na
kuwahadaa wananchi kuwa wana uwezo wa
kutatua kesi mbalimbali hali ambayo imekuwa
ikichochea migogoro mingi na hasa ardhi ambapo
amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua.
Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa
mkoa wa Kigoma Silvesta Kainda amesema idara
ya mahakama mkoa wa Kigoma imejipanga
kuhakikisha inatenda haki na kutatua kesi
mbalimbali zinazofunguliwa kwa wakati ambapo
nao mawakili wa kujitegemea wakizungumza
baada ya kutoa msaada kwa wagonjwa katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya siku ya sharia nchini
wamesema watakabiliana na watu wanaichafua
fani hiyo na kwamba bado wananchi wengi katika
mkoa wa Kigoma wanahitaji msaada wa kisheria
kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya
wanasheria.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post