Watu saba wameuwawa kinyama katika kipindi
cha miezi miwili maeneo mbalimbali ya jimbo la
Muleba kusini mkoani Kagera hali iliyosababisha
wananchi kuishi kwa hofu kubwa wakilalamikia
vyombo vya usalama kwa kushindwa kuwadhibiti
uhalifu.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la
Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka akiwa na
wabunge wa umoja wa katiba UKAWA katika
mazishi ya diwani wa kata ya Kimwani kupitia
chama cha wananchi CUF Bw.Silvesta Mringa
aliyeuwawa kinyama na kusababisha uvunjifu wa
amani huku wananchi wakichukua sheria
mikononi kwa kuteketeza kwa moto nyumba
nane, gari, mashine za kusaga nafaka na
kuhalibu baadhi ya mashamba ya watuhumiwa
ambapo jeshi la polisi linawashikilia watu 11
kutokana na matukio hayo.
Kufuatia hali hiyo chama cha wananchi CUF
kimelaani vikali mauwaji ya kinyama ya diwani
wa kata ya Kimwani Silvesta Mringa huku
wabunge wanaounda umoja wa katiba wa
UKAWA wakiahidi kutorudi bungeni hadi
watakapohakikisha watuhumiwa wa mauaji wote
wamekamatwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Muleba
Bw.Fransice Isack amewataka wananchi
kushirikiana na serikali kuwafichua wahalifu
waliopo kwenye maeneo yao kwa lengo la
kudhibiti uhalifu unaotishia amani katika wilaya
ya Muleba.
Marehemu Silvesta Mriga diwani wa kata ya
Kimwani aliyeuwawa kinyama ameacha mke na
watoto 13 Bwana alitoa na sasa ametwa kwa
kuwa amempenda zaidi yetu.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon