Serikali yapiga marufuku uuzwaji wa chakula nje ya nchi bila kuweka akiba mkoani Kilimanjaro.

Serikali mkoani Kilimanjaro impiga marufuku
uuzwaji wa mazao ya chakula nje ya nchi bila
kuweka akiba ya kutosha ili kukabiliana na tatizo
la njaa ambalo limeanza kukumba baadhi ya
mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Amos Makala
ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa zoezi la
upandaji miti zaidi ya 200 katika eneo la hifadhi
ya mlima Kilimanjaro katika msitu wa Nusus Mail
wilayani Rombo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mbomai
baada ya zaoezi la upandaji miti na kutembelea
mashamba ya wakulima mkuu huyo wa mkoa
ameagiza uongozi wa wilaya kuhakikisha
wananchi wanaweka akiba ya chakula cha
kutosha na kuuza ziada kutokana na wananchi
wa wilaya ya Rombo kubainika kuuza mazao ya
chakula nchi jirani ya Kenya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rombo
Bw. Lembris Kipuyo amesema hali ya uzalishaji
wa chakula katika wilaya ya Rombo mwaka huu
inaridhisha na kwamba kila familia imetakiwa
kuweka akiba ya magunia 10 ya chakula.
Baadhi ya wakulima katika wilaya ya Rombo
wanalalamikia ucheleweshwaji wa pembejeo za
ruzuku ambazo zinawafikia baada ya msimu wa
kilimo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post