Watanzania watakiwa kutii katiba na sheria za nchi.

Watanzania wametakiwa kuhakikisha wanatii
katiba Tanzania na sheria za nchi bila
kushurutishwa ili kuweza kuishi kwa amanai na
usalama.
Katibu tawala wa mkoa wa Singida Bwana
Phesto Kangombe amesema hayo kwenye
mwendelezo wa wiki ya ulimishaji wa sheria
mkoani Singida na kuwataka watanzania
kuhakikisha wanaitumia wiki hii kupata elimu ya
kisheria ili kuweza kuwasaidia kufahamu sheria
mbalimbali na kuwa katika usalama zaidi.
Awali hakimu mkazi mfawidhi mwandaminzi wa
mkoa wa Singida Bi Joyce Ninde amesema
wameandaa idara mbalimbali zinazo husiana na
maswala ya sheria wiki nzima kutoa elimu kwa
wananchi.
Maadhimisho ya siku ya sheria mwaka huu yana
kauli mbiu isemayo huduma za haki kumlenga
mwananchi,wajibu wa mahakama na wadau.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post