Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC
kimemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa
huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta
uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila
kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya
kusimamia na kuongoza tume hiyo.
Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na
kaimu mkurugenzi mtendaji wa LHRC Bi Imelda
Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi
na rasimi za michakato ya maridhiano toka
kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya
wananchi juu ya viongozi wao, tume na
mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia
Zanzibar.
Wakati huohuo chama cha kijamii CCK
kimemsimamisha kazi na uanachama naibu
katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Ali
ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar
kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC
Oktoba 2015.
Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda
amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili
kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi
wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK
itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar
kinyume na taratibu za chama.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon