Wanafunzi Butiama watumia viwanja vya mpira kusomea kutokana na uhaba wa madarasa.

Watoto zaidi 1,194 ambao wameandikishwa
kuanza darasa la kwanza mwaka huu katika shule
tano za msingi ndani ya kata ya Kianyari wilayani
Butiama mkoani Mara wanalazimika kutumia
viwanja vya michezo kama madarasa baada ya
shule hizo kukabiliwa na upungufu mkubwa wa
vyumba vya madarasa.
Akizungumza katika kikao cha maendeleo ya kata
ya Kianyari, mratibu wa elimu kata hiyo Bw
George Bigori, amesema wastani ya watoto mia
moja hadi mia tatu wameandikishwa kuanza
darasa la kwanza kwa kila shule ya msingi
katika kata kianyari, idadi ambayo amesema
imekuwa kubwa ukilinganisha na vyumba vya
madarasa vilivyopo.
Hata hivyo mratibu huyo wa elimu katika kata
hiyo ya Kianyari, amesema kuwa pamoja na
wazazi kutakiwa kuchukua hatua zinazolenga
kupunguza baadhi ya changamoto katika shule
hizo, lakini pia halmashauri ya wilaya ya Butiama
kupitia idara ya elimu imetangaza kuchukua
hatua kali kwa walimu wakuu ikiwa ni pamoja na
kuwavua nyadhifa zao endapo itabaini kuna
mwanafunzi amefika darasa la tatu bila kujua
kusoma, kuandika na kuhesabu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post