Wananchi wa kijiji cha Nanjalu wilayani Ruangwa wanaishi kwa kula matunda Porini.

Hekari zaidi ya 545 za mahindi na mpunga
zilizoko katika kijiji cha Nanjulu tarafa ya
mandawa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi
zimesombwa na maji kufuatia mafuriko yaliyo
sababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha
ambapo kaya 231 zinaishi katika maisha ya shida
na kula matunda ya porini aina ya mbilimbi kama
chakula cha kuwafanya waendelee kuishi.
Nihali isiyo ya kawaida kwa wahanga hao baada
ya mtafiti wa kituo cha utafiti wa mazao jamii ya
mizizi cha naliendele kutoa sampu ya shina la
Mhogo kwa mkuu wa wilaya ya Ruwangwa
Bi.Mariamu Mtima nakuamua kuwapa akina
mama moja na jingine akina baba wagawane
matarajio yake yalikatishwa ghafla na kile kilicho
daiwa kuwa ni njaa na kuanza kunyang’anyana
Mhogo huo ambapo wameiomba serikali
kuwatazama kwa jicho la tatu kwani maisha yao
yamekuwa wakiishi kwa kula matunda ya porini.
ITV na wahanga hao wakiwemo viongozi wa
taasisi ya utafiti na maendeleo naliendele
wametembelea maeneo yalipo kuwa mashamba
hao nakukuta mazao yamesombwa na maji
ambapo mratibu mazao jamii ya mizizi kitaifa
Daktari Geoffrey Mkamilo amesema imewalazimu
kupeleka mbegu hizo zinazozaa kwa mdamfupi ili
wahanga hao wapate kujikwamua kimaisha
baada ya miezi miwili ijayo kuanzia sasa.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima
akipokea mbegu hizo ameshukuru kituo cha
mbegu cha naliendele kwakutoa mbegu hizo
ambazo zitawafanya wahanga hao kurudi katika
hali ya kupata chakula kwa mda mfupi
sambamba na kuwataka vijana waache kucheza
pulu na bao badale yake walime iliwaondokane
na umasikini.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post