Serikali yawataka watendaji TRA kuacha kuwatisha wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa fedha na mipango Mh Dr. Philp
Mpango amesema hakuna mtendaji wa serikali
aliyejinufaisha na mapato ya serikali atakaye
samehewa na hakuna mtendaji mwadilifu
atakayeonewa.
Mh .Dr Mpango ameyasema hayo alipokuwa
anazungumza na watendaji wa kituo cha pamoja
cha forodha cha Holili mkoani Kilimanjaro.
Aidha amewataka maafisa wa TRA kukufanyakazi
kwa uadilifu na kuacha kutumia kampeni
zinazoendelea za kudhibiti mapato kuwatisha
wafanyabiashara badala yake wawasaidie
waweze kuzalisha na kulipa kodi halali.
Aidha amewataka watendaji wa mamlaka ya
mapato ambao bado hawajatangaza mali zao
wanazomiliki kufanya hivyo mara moja kwani
hakuna njia ya mkato lazima lengo la serikali la
kuisafisha mamlaka hiyo mbele ya jamii litimie.
Kuhusu malalamiko ya kuendelea kuwepo kwa
usumbufu wa baadhi ya watendaji wanaotumia
nyadhifa zao kuwasumbua na wasafirishaji wa
bidhaa na kuwawekea vikwazo barabarani Dr
Mpango amesema siku zao zinahesabika na
amewataka wananchi na watumishi wadilifu
kuwafichua kwani wanawasababishia watu
wengine matatizo.
Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro Bw Abdul
Mapembe amesema ukusanyaji wa mapato
unaendeleabkuongezeka siku hadi siku licha ya
kuwepo kwa baadhi ya changamoto ikiwemo ya
uhaba wa vitendea kazi.
Kwa sasa ukusanyaji wa mapato umeongezeka
kutoka bilion mia tisa hadi kufikia trilion 1.6 kwa
mwezi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post