NEC waanza kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC) imeanza
zoezi la kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu
uliofanyika mwaka jana 2015 unaolenga
kutambua mafanikio na changamoto zilizojitokeza
na kuanza kuzifanyia kazi zoezi litakalofanyika
katika kanda zote nchini likiwashirikisha wadau
mbali mbali zikiwemo asasi za kiraia.
Anakizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa
tume hiyo jaji mstaafu Damiani Lubuva, kamishna
wa tume hiyo Prof Amoni Chaligha amesema
miongoni mwa mambo yanayofanyika ni pamoja
na kuangali mchango wa wadau mbalimbali
wakiwemo wananchi katika kushiriki
nakufanikiksha uuchaguzi huo ukiwemo
uliotolewa na asasi za kiraia zilizokuwa
zimepewa jukumu la kutoa elimu ya uraia.
Baadhi ya wawakilishi wa taasisi hizo za kiraia
wamesema tatizo la ukosefu wa elimu ya uraia
na faida zake bado ni kubwa na wameitaka tume
kuhakikisha inakuwa ni agenda ya kitaifa na
itolewe wakati wote badala ya kusubiri wakati
wa uchaguzi.
Hata hivyo wawakilishi wa baadhi ya makundi
likiwemo la walemavu na wazee wamesema bado
hawajashirikishwa ipasavyo kutoa mchango wao
na wamesema asilimia kubwa ya wazee na
walemavu wa kusikia walishindwa kushiriki
uchaguzi kutokana na kutowekewa miundombinu
ya kuwawezesha kusikiliza sera za wagombea
wakiwemo wakalimani.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post