Walimu wakike wanakosa maadili ya mavazi- Msangi

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,
Bituni Msangi amesema kuwa baadhi ya walimu
wa kike nchini hawavai mavazi yenye maadili ya
ualimu hatua ambayo huwasababisha wanafunzi
hasa wa kiume kuwataka kimapenzi.
Msangi ambaye pia kitaaluma ni mwalimu
ametoa kauli hiyo kwenye hafla iliyoandaliwa na
Chama Cha Walimu (CWT) Wilayani Kongwa kwa
ajili ya kuwaaga walimu waliostaafu katika Wilaya
hiyo.
Amesema kuna baadhi ya walimu wa kike ambao
wamekuwa wakikiuka maadili kwa kuvaa mavazi
mafupi na ya kubana wawapo kazini hali ambayo
huwa inawanyima wanafunzi wa kiume utulivu wa
kujifunza ambapo amewaagiza maofisa elimu
kuwaeleza walimu wao namna bora ya uvaaji.
Katika hafla hiyo jumla ya walimu 17 waliostaafu
walipata zawadi ya mabati 20 kila mmoja
waliyopewa na chyama cha walimu Wilayani
humo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post