CUF msisusie uchaguzi jipangeni - BAKWATA DSM

BAKWATA Dar es salaam imetoa salamu hizo za
pongezi leo lilipokutana na vyombo vya habari, na
kusema kwamba hatua hizo zimeanza kuleta tija
kwa taifa kama inavyoshuhudiwa pato la serikali
linavyoongezeka,
“Kusudi kubwa la kuwaiteni leo ni kutaka kutoa
salamu za pongezi kwa serikali ya awamu ya
tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli,
kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua
zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa
watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza
kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo
tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali
likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh
alhadj Mussa Salum ambaye ndiye sheikh mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam.
Pia Baraza hilo limeipongeza serikali kwa kitendo
cha kubana matumizi na kuweka kipaumbele
huduma za jamii, kama suala la elimu bure.
“Aidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya
kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na
badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za
jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na
huduma hizo kama vile suala la elimu bure”,
alisema Sheikh Salum.
Vile vile Baraza hilo limeitaka serikali
kushughulikia changamoto za jiji la Dar es
salaam ikiwemo tatizo la foleni, kwani
linazorotesha uchumi pale wafanyakazi
wanapochelewa sehemu zao za kazi, na kuomba
kuanza kutumika kwa mabasi ya mwendo kasi ili
kupunguza tatizo hili.
Pamoja na hayo Baraza hilo limeongelea suala la
Zanzibar huku likisema ninaunga mkono uamuzi
wa ZEC, na kukiomba chama cha CUF kukubali
kurudia uchaguzi, ili kutatua mgogoro huo.
“Kuhusiana na suala la mgogoro uliopo Zanzibar,
sisi BAKWATA MKOA WA DAR ES SALAAM,
tunaunga mkono uamuzi wa Tume ya uchaguzi
Zanzibar (ZEC) kuamua kufanya uchaguzi wa
marudio, hivyo basi naomba kuchukua fursa hii
kukiomba chama cha Wananchi CUF ambacho
kimeshatangaza kususia uchaguzi huo, viache
kususia uchaguzi huo bali vijipange na kushiriki”,
alisema Sheikh Salum.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post