Walimu wa serikali manispaa ya kinondoni kutolipa nauli kwenye daladala.

Chama cha wamiliki wa daladala jijini Dar es
Salaam-Darcoboa- kwa kimepanga kuhacha
kuwatoza walimu wote wa shule za msingi na
sekondari za serikali katika manispaa ya
Kinondoni kuanzia machi 7 mwaka huu ikiwa ni
kuungamkono uamuzi wa rais Dkt John Magufuli
wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya
msingi na sekondari.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari, mwenyekiti wa Darcoboa Bwana Said
Mabrouk amesema walimu wa shule za msingi na
sekondari za serikali hawatotoza nauli kuanzia
saa 11 alfajiri hadi saa 2 asubuhi na wakati wa
mchana ni kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni, na
kusisitiza ambapo ametaka hamalshauri za
manispaa kuweka utaratibu maalum wa
vitambulisho vitakavyokuwa na picha za walimu
hao.
Aidha akizungumza katika mkutano huo,
mwenyekiti wa umoja wa wasafirishaji mkoa wa
Dar es Salaam Bwana William Masanja
amevitaka vyombo vya habari kutoa ushirikiano
wa kutangaza mpango huo wa wamiliki wa
daladala, umoja wa wasafirishaji, chama cha
wafanyakazi madereva-Tadwu na serikali ili
kuwawezesha walimu kufahamu wa shule za
serikali kutambua fursa hiyo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post