Polisi apigwa risasi siku yake ya kwanza kazini

Polisi mmoja wa kike nchini Marekani amepigwa
risasi na kuuawa katika siku yake ya kwanza
kazini.
Askari huyo bi Ashley Guindon alikula kiapo
mapema siku hiyo hiyo kisha akaelekezwa na
wakubwa wake kwenda nyumbani kwa mama
mmoja kutatua mzozo wa kinyumbani katika
kitongoji Washington, DC.
Bi Ashley akiandamana na wenzake wawili
walikwenda Woodbridge, Virginia, kilomita 32
kusini mwa Washington lakini walipofika huko
walifyatuliwa risasi na kwa bahati mbaya Ashley
hakubahatika.
Wenzake wawili pia walijeruhiwa vibaya na
wamelazwa hospitalini.
Mshukiwa wa mauaji hayo ni mlengaji shabaha
katika jeshi la Marekani aliwazidi maarifa
maafisa hao wachanga.
Mwanjeshi huyo alikamatwa baadaye na vitengo
maalum vya polisi.
Mwanjeshi huyo alikuwa amempiga risasi na
kumuua mkewe papo hapo kabla ya Ashley na
wenzake kutokea.
Hakukuwa na mtoto nyumbani wakati wa
ufyatulianaji huo wa risasi.
Afisa mkuu wa kituo " Tunasikitika kuwatangazia
kifo cha afisa wa polisi wa kituo cha Prince
William County bi,Ashley Guindon, aliaga dunia
kufuatia ufyatulianaji risasi katika mtaa wa
Lashmere Ct akiwa kazini.
Mapema siku hiyo hiyo kituo hicho kilikuwa
kimetoa picha ya afande huyo kwenye mtandao
wa Twitter ikimkaribisha kwa huduma kwa wote.
''Tunafurahi kuwakaribisha afande Ashley
Guindon na mwenzake kwa huduma kwa wote''

Previous
Next Post »

Ads Inside Post