Kamishna wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na
Ufundi, Profesa Eustella Bhalalusesa
amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu
Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua
madaraka Wakuu Watatu wa vituo vya
Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka
utaratibu wa kuchagua wanafunzi
wanaojiunga kidato cha kwanza na
kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu
Wazima.
Profesa Eustella amesema kukiukwa kwa
utaratibu huo kumesababisha hali ya
sintofahamu kwa wazazi hasa katika kipindi
hiki cha utoaji wa Elimu bure.
Kamishna wa Elimu Tanzania amesema
kuwa, wakufunzi hao wamekuwa
wakishirikiana na Halmashauri baada ya
kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza
ambao wamefanya vizuri, wao huchukua
waliofeli na kuwapeleka katika shule za
serikali wakidai kuwa wamechaguliwa katika
chaguo la pili.
Kamishina wa Elimu pia amemtaka
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu
wazima huyo kuweka mikakati ya
kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya
urtaratibu wa kuchagua wanafunzi wa
taasisi hizo ilikiwemo suala la malipo.
Amesema wakufunzi hao wamekuwa
wakichukua matokeo ya kidato cha kwanza
kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati
wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu
wazima ni hiari kutokana na sera ya elimu.
Aidha Wizara ya Elimu imewataka
wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa kwa
wizara pindi wanapokutana na changamoto
za elimu, lengo likiwa ni kuhakikisha
wanafunzi wanapata elimu bora.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon