Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania
TMF umepunguza idadi ya waandishi
watakaopewa ruzuku mwaka 2016 kutoka
waandishi wa habari 200 hadi 85 lengo
likiwa ni kupata kazi zilizo bora zaidi na
zitakazoleta mabadiliko ya uwajibikaji.
Punguza hilo limeelezwa kuwa litasaidia
kuwepo kwa usimamizi makini kwa
waandishi wa habari watakaopewa ruzuku
pamoja na kujifunza zaidi ili kufanya kazi
zitakazoleta mabadiliko katika jamii.
Hayo yameelezwa katika kikao cha
majadiliano baina ya waandishi wa habari
na mfuko wa vyombo vya habari nchini,
kikao ambacho kimelenga kutoa muongozo
juu ya ruzuku zitakazotolewa na mfuko huo
katika mwaka huu .
Katika kikao hicho Mkurungezi TMF Ernest
Sungura amesema idadi ya waandishi
watakaodhaminiwa na mfuko huo kwa ajili
ya andiko la mradi wa kihabari kwa mwaka
2016 kutoka waandishi wa habari 200 hadi
85 lengo likiwa ni kupata kazi zilizo bora
zaidi na zitakazoleta mabadiliko ya
uwajibikaji.
TMF imesema safari hii watazingatia
mashariti ya kimkataba na waaandishi
watakaopewa ruzuku kutoka katika mfuko
huo, na wale watakaokiuka wataondolewa
udhamini wa ruzuku waliyopewa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon