Matokeo ya kidato cha Nne na Taarifa Yake

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji
wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde
amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947
sawa na 67.53% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015
wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo
ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa
watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996
sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya
mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84)
na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa
shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85
ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa
kujitegemea, Dkt Msonde amesema
watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80
wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa
29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa
kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa
wa shule, Msonde amesema waliopata
daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia
2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na
asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa
na asilimia 13.56.
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996
sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja
la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na
asilimia 32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati
ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941
sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa
56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338
sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa
masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu
wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili
ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku
ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la
Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76
wamefaulu.
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo
wa madaraja (Division) badala ya ule wa
wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo
iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post