Wahamiaji 39 raia wa Ethiopia walioingia nchini bila kibali wakamatwa mkoani Kilimanjaro.

Wahamiaji haramu 39 raia wa Ethiopia
wamekamatwa wilayani Mwanga mkoa ni
Kilimanjaro baada ya kuingia nchini kinyume cha
sheria kupitia mpaka wa Tarakea Rombo wakiwa
na nyakara feki za kusafiria kama raia wa
Somalia.
Afisa uhamiaji wa mkoa wa Kilimanjaro DCI
Ebrocy Mwanguku amethibitisha kukamatwa kwa
wahamiaji haramu hao katika kituo cha ukaguzi
barabarani wakisafirishwa na watu watano wenye
asili ya Kimasai kwa kutumia usafiri wa magari
madogo aina ya Toyota Noah, na Toyota Starlet
katika eneo la wilaya ya Mwanga na majengo
mjini Moshi.
Amesema wahamiaji hao wamekamatwa kwa
ushirikiano wa maafisa wa uhamiaji na jeshi la
polisi na kuwataka wananchi mkoani Kilimanjaro
kutoa taarifa za uwepo wa watu wanaowatilia
mashaka katika maeneo yao hususani mipakani ili
hatua za kisheria zichukuliwe mapema.
Mmoja wa wahamiaji haramu hao ambaye
amejulikana kwa jina la Debede mwenye uwezo
wa kuzungumza lugha ya kiingereza amesema
wametokea nchini Ethiopia na kwamba wamepitia
Tanzania kuelekea nchini Afrika ya Kusini huku
mmoja wa watumiwa waliokuwa wanawasafirisha
Bw. Baraka Laizer akisema alipewa taarifa za
kupokea wageni hao kwa ajili ya kusafiri kueleka
mkoa wa Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
Bw.Ramadhani Mungi amesema wahamiaji
haramu ni hatari na kwamba katika kipindi cha
kuanzia mwezi January mwaka huu jumla ya
wahamiaji haramu 79 wameakamatwa katika
maeneo mabalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post