Polisi mkoani Mara yawakamata watu saba kwa kubaka na mauaji ya mtoto.

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu
saba kwa tuhuma za kumbaka kisha kunyongwa
hadi kufa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
minne na nusu Mariam Deaogratus ambaye
aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya awali ya
makoko katika manispaa ya Musoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna
msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex
Kalangi, amesema watu hao wamekamatwa siku
moja tu baada ya kutokea kwa tukio hilo la
kikatili.
Awali kamanda alisema mtoto huyo alikumbwa
na mkasa huo muda mfupi baada ya kuondoka
nyumbani kwao jioni ya Februari 23 mwaka huu
kwenda shule kwa ajili ya masoma ya ziada,
lakini akuonekana tena hadi saa 2 usiku wa siku
hiyo Februari 23, mwili wake ulipokutwa
ametupwa katika nyumba ambayo ujenzi wake
unaendelea.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama wilaya ya Musoma, kamishina
mwandamizi mstaafu wa jeshi la polisi Zeloth
Stephen, amesema vyombo vya dola vitafanya
kila Nnjia katika kuhakikisha mtu yoyote ambaye
amefanya kitendo hicho cha kikatili anakamatwa
na kufikishwa mara moja katika vyombo vya
sheria.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post