Waalimu Kahama wapaza sauti zao kuitaka serikali itatue changamoto za kielimu.

Mlundikano wa wanafunzi wengi katika darasa
moja unatajwa kusababishwa na utelekezaji wa
sera ya elimu bure huku miundombinu ikiwa finyu
hali ambayo imeanza kuathiri shule za wilaya ya
Kahama na kuwaweka walimu kwenye wakati
mgumu unaotokana na ongezeko kubwa la
wanafunzi katika shule za msingi na sekondari.
Walimu wa shula za msingi na sekondari wilaya
ya Kahama katika mkoa wa Shinyanga wametoa
kauli hiyo walipokuwa wanazungumza na ITV na
kudai kuwa zoezi linalo tekelezwa na serikali bila
marekebisho ya miundombinu na vitendea kazi
katika shule za msingi na sekondari limewaweka
katika wakati mgumu hali inayoweza kurudisha
nyuma jitihada za kutoa elimu bora kwa
wanafunzi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya
la ofisi ya chama cha walimu wilayani kahama
rais wa chama hicho Bw.Gratian Mukoba
amsema serikali isiporekebisha mazingira na
miundombinu katika shule zake kulingana na
ongezeko la wanafunzi elimu ya tanzania
itashuka kiwango na malengo ya elimu bure
hayatafanikiwa kama ilivyodhaniwa na wengi
huku mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vita
Kawawa akidai kuwa serikali inazitambua
changamoto za walimu na inaendelea kuzitatua
kwa awamu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post